KIPINDI CHA RADIO "NG'ANG'ANIA" TOP FM
Kwa neema ya Mungu, miaka kama kumi iliyopita Tanzania iliweza kuingia kwenye hatua nyingine ya kimaendeleo pale sheria ilipopitishwa kuruhusu watu binafsi kufungua vituo vya televisheni na radio, ambapo serikali ilianza kutoa vibali vya kumiliki masafa ya kurushia matangazo. Kwa neema hii vyombo vya habari vya kikristo vilivyo chini ya madhehebu au chini ya mwamvuli wa huduma vilipata fursa ya kufungua vituo hivi. Japokuwa, pamoja na kuwa na vyombo hivi vya habari vinavyomilikiwa na makanisa mbalimbali lakini bado gharama za matangazo ni kubwa, hata pale ambapo watangazaji wanapokuwa ni makanisa, huduma au watumishi wanaomtumikia Mungu katika roho na kweli; hii imeendelea kulifanya zoezi la kutelekeza utume mkuu wa Yesu badala ya kuurahisisha umeendelea kufanywa mgumu. Lakini hata hivyo, kwa kuwa kanisa la Maranatha Reconciliation linaamini zaidi miujiza zaidi ya hali halisi iliyopo, kupitia mtumishi wa Mungu Askofu Rodrick Mbwambo, liliamua kujikita katika kueneza injili ya Yesu Kristo kwa njia ya matangazoa ya Radio bila kujali ukubwa wa gharama. Tayari kanisa limeanza kurusha kipindi cha injili kupitia radio ya Kikrsito inayojulikana TOP FM ya mjini Morogoro, Tanzania kila wiki mara moja. Katika kipindi hiki ambacho hurushwa hewani na kuruhusu maswali ya moja kwa moja, kimeleta matokeo makubwa yanayoashiria kiu kubwa ya watu kufunguliwa na kupokea miujiza yao. Mafundisho yanayotolewa na Askofu Rodrick Mbwambo, kwa hakika ni ya kipekee sana kwa kuwa haambatana na nguvu ya Mungu. Utakapoendelea kusikiliza mafundisho haya kwa moyo wa dhati hutakuwa kama ulivyokuwa tena! KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU KIPINDI HICHO UTAPEWA KUANZIA WIKI IJAYO. |
![]() |
Kuhusu Huduma
- Sisi ni nani?
- Nini tunachokifanya
- Ndani ya Kanisa la Maranatha
- Umisheni: Tanzania & Africa
- Maoni yako
AGIZA JARIDA LA
NG'ANG'ANIA BURE
|
![]() |
-
Usoma Shuhuda za matendo makuu ya Mungu. Makala za neno la Mungu pamoja na mafundisho ya Askofu Rodrick Mbwambo bila kusahahu mafundisho yenye nguvu na Mch. Belobaba wa Marekani.
Na Habari mbalimbali utazipata ndani ya jarida la Ng'ang'ania














