NUNUA VITABU, AUDIO CD, DVD NA MACHAPISHO MENGINE HAPA
Ili kuupa ulimwengu mkate ulio kamili, kanisa la Maranatha Reconciliation, limeweka mafundisho na mahubiri yake katika vitabu, kanda, CDs na vipeperushi. Kwa yeyote anayehitaji funzo la aina yoyote ile anaweza kuagizia kwa kutumia anwani katika ukurasa huu.
VIPEPERUSHI
Pamoja na vitabu hivi, tunavyo vipeperushi kwa ajili ya uinjilisti wa maandiko. Vipeperushi tulivyo navyo ni pamoja na Ukimwi usiniue, Simu kutoka kuzimu, Kutoka Positive hadi Negative na upagani wa kisasa. Kama wewe ni miongoni mwa wale wanaovunia Bwana kwa njia ya uinjilisti wa maandiko, hakikisha kuwa unajipatia hazina ya kutosha ya vipeperushi hivi.
KANDA ZA KASETI NA CD Tunayo mamia kwa mamia ya kanda za mafundisho kwa kila fundisho unalohitaji. Unachotakiwa kufanya, ni kuomba orodha ya kanda na CD zilizopo katika maktaba zetu.
Kama unahitaji kununua vitabu hivi, (Kwa nchi za Afrika Mashariki tu) tafadhali tutumie ANWANI YAKO KAMILI YA POSTA PAMOJA NA FEDHA KWA AJILI YA KITABU/VITABU na GHARAMA ZA UTUMAJI. Na kama utapenda kutumia njia za UPESI (Courier Services) kama EMS au DHL tujulishe, nasi tutakupa gharama zao za utumaji vifurushi. Lakini njia ya nafuu kuliko hizo zingine ni POSTA. Kwa POSTA ongeza Tshs 300/= kama ada ya kutuma kitabu kimoja. Kwa vitabu vingi, baada ya siku chache zijazo tutaambatanisha gharama za utumaji vitabu kulingana na idadi mbalimbali. Anwani yetu ni hii: Maranatha Reconciliation Church, P.O. Box 7812, Dar es Salaam, Tanzania. Au tuandikie kwa kutumia e-mail yetu: maranathainfo@maranatha-upendo.org au kwenye orodha utaona kitufe kimeandikwa "Agiza." Bonyeza hicho kwa ajili ya kutoa oda ya kitabu au vitabu, au vipeperushi vya injili au kanda mbalimbali. Vitabu Vilivyopo kwa sasa kwenye ukurasa huu ni pamoja na hivi vifuatavyo (orodha nyingine itafuata):-
HUDUMA YENYE THAWABU Hiki ni kitabu cha waamini walio na uti wa mgongo wa kiroho uliokomaa, waamini waliojifunza kusimama kwa miguu yao wenyewe. Ni kitabu cha watu walioingia katika zoezi la kuandaa makao na taji zao, katika ulimwengu ujao. Kinaelezea jinsi ya kumnyang’anya Shetani mateka, kisha kuyaandaa mateka hayo kuwa mawe yaliyo hai katika hekalu la Mungu. Kama wewe ni miongoni mwa wale wanaotaka kuingia mbinguni kwa kishindo, usikubali kukikosa kitabu hiki. RODRICK MBWAMBO
MAISHA YA USHINDI Kama vile Kristo alivyoishi maisha ya ushindi alipokuwa katika mwili hapa duniani, nawe pia unayo nafasi ya kuishi maisha ya ushindi. Kitabu kinachoweza kukusaidia kufanikisha ndoto yako ya kuishi maisha ya ushindi, ni kitabu hiki cha Maisha ya ushindi. Ni kitabu maalum kwa yule anayetaka kumliza Ibilisi na kuifurahisha mbingu. Kitabu hiki kitakusaidia kula na kunywa huku maadui zako wakikutazama. RODRICK MBWAMBO
NIMEOKOKA, NIABUDU WAPI? Hiki ni kitabu kilicholenga kuwakinga waamini dhidi ya imani kengeufu, zinazotenda kazi katika kizazi chetu. Kama unavyoelewa, hakuna miaka ambayo kanisa la Mungu limevamiwa na imani kengeufu kama ilivyo katika siku hizi za mwisho. Baada ya miaka mingi ya kupambana na waalimu wa uongo na imani kengeufu, Askofu Rodrick Mbwambo, anakuonyesha jinsi ya kulitambua kanisa la kweli linalofaa kukulea kiroho. Kama kiroho chako kimefikia kiwango cha kuwa mhimili unaoegemewa na wengine, unakihitaji kitabu hiki ili uwasaidie wale wote wanaoutegemea ushauri wako. RODRICK MBWAMBO
ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE Maneno ya mwisho ya Yesu kwa wanafunzi wake kabla ya kupaa yalikuwa, “Mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu.” Matendo 1:8. Kitabu hiki kinakueleza jinsi ya kumpokea Roho Mtakatifu, ishara ya kunena kwa lugha, kazi za Roho Mtakatifu na jinsi ya kutembea naye. RODRICK MBWAMBO
MNADHIRI WA MUNGU Kinamwelezea kila mwamini kama mnadhiri wa Mungu na mambo yanayoweza kumzuia Mungu kutenda kazi katika maisha yake. Kama umedhamiria kumwona Mungu baada ya maisha haya, hutataka upitwe na kitabu hiki. RODRICK MBWAMBO
KUSIKIA KUTOKA KWA MUNGU Katika Biblia uhusiano kati ya kanisa na Mungu, unalinganishwa na ule wa baba kwa watoto wake. Mungu kama Baba, anatamani kila wakati kuongea na watoto wake, kama vile alivyofanya kwa Musa. Biblia inasema kuwa, Musa aliongea na Mungu, kama vile mtu anavyosema na rafiki yake. Kutoka 33:11. Kama unataka kuielewa sauti ya Mungu na kuongea naye, fanya hima upate kitabu hiki. RODRICK MBWAMBO
MASHAHIDI WAWILI WA UFUNUO Ukisoma katika kitabu Ufunuo wa Yohana, utakutana na mambo makubwa ya kutisha, yatakayotokea duniani baada ya kunyakuliwa kwa kanisa. Katikati ya dhiki hii, maandiko yanasema kuwa, watatokea mashahidi wawili hali wamevaa nguo za magunia! Ufunuo 11:2-12. Kulingana na maandiko, katika vinywa vya watu hawa, kutatoka moto ulio na uwezo wa kuangamiza chochote kinachoinuka kinyume na huduma yao. Kama unataka kuwa na kinywa kilicho na maneno yenye nguvu za kufanya mambo makubwa, agiza kitabu hiki. RODRICK MBWAMBO
JINSI YA KUSHINDA MAJARIBU Yesu Kristo alipokuwa akielezea matatizo yaliyopo duniani, aliwaambia wanafunzi wake kuwa, “duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo, kwa kuwa mimi nimeushinda ulimwengu.”Yohana 16:33. Yesu alishinda majaribu kwa kuwa, alifahamu jinsi ya kupambana na majaribu hayo. Kama unapitia majaribu mazito kama moto, kitabu hiki kitakutoa kwenye bonde la machozi na kukupeleka kwenye bembea ya furaha na shangwe. RODRICK MBWAMBO
BEI: TSHS 1500/=
ORODHA YA VITABU VINGINE NA KANDA IKO MBIONI KUJA KWENYE UKURASA HUU
Usoma Shuhuda za matendo makuu ya Mungu. Makala za neno la Mungu pamoja na mafundisho ya Askofu Rodrick Mbwambo bila kusahahu mafundisho yenye nguvu na Mch. Belobaba wa Marekani.
Na Habari mbalimbali utazipata ndani ya jarida la Ng'ang'ania
Jesus is Lord and Savior
SHUHUDA ZA AJABU
MIUJIZA HAPA
Kwa miaka zaidi ya 20 kanisa la Maranatha Reconciliation limekekuwa likimwakilisha Yesu Kristo kwa kutekeleza agizo kuu la utume alilotuachia, ambapo pamoja na kuhubiri Injili limekuwa likiombea watu walioonewa na shetani kwa kuponya magonjwa, kutoa pepo na nguvi zote za. SOMA SHUHUDA HAPA.
Kwa mawasiliano
Usisite kuwasiliana nasi wakati wowote kwa kutumia anwani na simu zifuatazo:-
Posta: P.O. Box 7812, Dar es Salaam Simu: +255 719 310021 Others: +255 655 855 553 Email: maranathainfo@maranatha-upendo.org