SAA YA MUUJIZA WAKO NI SASA!



HAKUNA JAMBO ASILOLIWEZA MUNGU TANGU ALIPOZIUMBA MBINGU NA NCHI. ALISEMA
NENO, DUNIA IKAUMBWA. ALISEMA NENO, JUA LIKAUMBWA. ALISEMA NENO, CHAKULA KIKAUMBWA. NA WAKATI YESU ALIPOKUWA DUNIANI, ALISEMA NENO, WAGONJWA
WAKAPONA. NA HUYU YESU, LEO ANAENDELEA KUTENDA MIUJIZA! AHADI ZAKE ZOTE NI KWELI. AKISEMA UTAPONA, NDIVYO ITAKAVYOKUWA.
LEO UTAWEKWA HURU! - Shalom Prayer Group


SOMA SHUHUDA ZA MATENDO MAKUU YA MUNGU HAPA

Mojawapo ya nguzo zinazolisimamisha kanisa la Maranatha Reconciliation na makanisa mengine ya watu wa Mungu, ni maombezi. Maombezi, ndiyo yanayolifanya kanisa la Kristo, liendelee kudumu katika kuyafanya mapenzi ya Mungu. Huduma hii ya maombezi katika makanisa ya Upatanisho ya Maranatha, iko wazi kwa mtu yeyote anayehitaji msaada kutoka kwa Mungu.

Maombi katika idara hii, huendeshwa na watu wanaoupenda mwili wa Kristo na waliojiweka wakfu kwa ajili ya huduma hii. Kwa kuwa maombezi yanahusika na siri za watu, maombi yote yanayopokelewa katika idara hii, hushughulikiwa kwa siri bila kutolewa kwa mtu yeyote. Hali kadhalika, baada ya maombi kujibiwa, majibu hayatatangazwa kwa mtu yeyote hadi pale mhusika, atakapotoa kibali. Uwajibikaji huu katika kuomba na kutunza siri za watu, ndio unaoifanya idara hii kukimbiliwa na maelfu ya watu ndani na nje ya Tanzania, wanaohitaji kupelekwa mbele za kiti cha enzi cha Mungu.

Kama wewe ni miongoni mwa wale wanaolia usiku na mchana kutokana na mwiba unaoyasonga maisha yako au ya familia yako, iletee timu hii ya maombi mahitaji yako. Unaweza kufanya hivyo kwa kujaza fomu ya maombi na kuituma kwetu kwa njia ya barua pepe, fax, simu au posta.

 

FOMU YA MAOMBEZI
*maeneo ambayo ni lazima yajazwe

Jina la Kwanza* Cheo
Jina la Mwisho*
Umri
Sanduku la Barua
Nchi
Jiji/Code*
Barua Pepe *
Mfano: mimi@maranatha-upendo.org
Simu Mezani au Mkononi

Mfano: 255-22-820190 (ya mezani) au 255-752-016037 (ya mkononi)
Umeoa/Olewa
(Kama jibu nni NDIYO, eleza kwenye kiboksi hiki kulia, kama ndoa hii ilipata indini ya wazazi na kama ni ya Kikristo)
Dhehebu linalokulea kiroho
Je umewahi kusikia habari za wokovu?

Kama jibu ni NDIYO, je umempokea YESU KRISTO kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako? Kama jibu lako ni NDIYO ni lini ulipookoka?
Je umebatizwa kwa Roho Mtakatifu, na ishara ya kunena kwa lugha?

Kama jibu ni NDIYO ni lini ulipoupokea ubatizo huo?
Je kuna mtu aliyekufanyia ubaya ambaye bado hujamsamehe?

Je kuna mtu uliyemfanyia WEWE ubaya lakini hujui kama amekusamehe au la?


Kama jibu ni NDIYO, je ni rahisi kumpata mtu huyo? Jibu NDIYO au HAPANA
ZINGATIA: Ikiwa kuna jambo lingine unalotaka tulifahamu kuhusu historia yako ya siku za nyuma, uwe huru kutuelezea.
TAJA HITAJI LAKO SASA kwa kuleleza mwaka lilipoanza na juhudi zozote, kama zipo, ulizafanya katika kukambana na tatizo hili, katika hili eleza kama ulishawahi kuombewa au kwenda hospitali au kwa waganga (mafundi).
JAZA HAPA HITAJI/MAHITAJI YAKO YA MAOMBEZI*
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Events Rodrick2 Pokea muujiza

Jesus is Lord and Savior

SHUHUDA ZA AJABU
MIUJIZA HAPA

Kwa miaka zaidi ya 20 kanisa la Maranatha Reconciliation limekekuwa likimwakilisha Yesu Kristo kwa kutekeleza agizo kuu la utume alilotuachia, ambapo pamoja na kuhubiri Injili limekuwa likiombea watu walioonewa na shetani kwa kuponya magonjwa, kutoa pepo na nguvi zote za. SOMA SHUHUDA HAPA.

Kwa mawasiliano

Usisite kuwasiliana nasi wakati wowote kwa kutumia anwani na simu zifuatazo:-

Posta: P.O. Box 7812, Dar es Salaam
Simu: +255 719 310021
Others: +255 655 855 553
Email: maranathainfo@maranatha-upendo.org

© Copyright Maranatha Reconciliation Church (MRC), Tanzania Design by Integrity Marketing Communications