HUDUMA YA KANISA LA MARANATHA RECONCILIATION

Bishop

Kanisa la Maranatha Reconciliation, ni tunda la huduma isiyofungana na dhehebu lolote iliyokuwa ikijulikana kama Maranatha Evangelistic Team International (MET). Huduma hii iliyoanzishwa mwaka 1990 na Askofu Rodrick Mbwambo, kwa lengo la kuhubiri na kufundisha neno la Mungu. Baada ya miaka saba ya kushirikiana na makanisa mbalimbali katika huduma hii, ulionekana umuhimu wa kuongeza huduma ya upandikizaji wa makanisa ndani ya MET. Kutokana na uhitaji huu, tarehe 28 Oktoba mwaka 1997, huduma ya MET ilibadilika kuwa kanisa linalojitegemea la Maranatha Reconciliation (MRC).

Jina la kanisa hili, limetengenezwa na maneno mawili ya lugha ya Kiaramu na Kingereza. Neno ‘maranatha’, ni la Kiaramu lenye maana ya, “Bwana anakuja.” 1 Wakorintho 16:22. Reconciliation ni neno la Kingereza, linalomaanisha upatanisho. 2 Wakorintho 5:18. Kutokana na maana ya maneno haya mawili, tunaweza kusema kuwa, MRC, ni ushirika wa watu wa Mungu, unaofuata mfumo wa kipentekoste, ulio na jukumu la kuuandaa ulimwengu tayari kwa parapanda ya mwisho. Mambo ya msingi yanayofanyika katika huduma hii ni pamoja na kuhubiri, kufundisha, kupandikiza makanisa na kuwahudumia maskini. Kutokea mjini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya kanisa hili, tayari makanisa yasiyopungua 50 yamepandikizwa katika mikoa kumi na tatu ya Tanzania.

Kwa sasa MRC chini ya uongozi wa askofu Rodrick Mbwambo, linafanya huduma zake kupitia idara zifutazo:- idara ya mafunzo na chuo cha Biblia, Yatima na Wajane, idara ya maandiko, idara ya uinjilisti, umisheni na uwakili, idara ya vijana, idara ya kinamama na watoto, idara ya msamaria mwema, idara ya kuwafikia makahaba ijulikanayo kama, ‘operation Rahab’, idara ya kuwafikia wafungwa, idara ya mafunzo mashuleni, idara ya ushauri, idara ya afya, idara ya miradi midogo midogo na idara ya michezo.

 

TAMKO LA IMANI

1. Linaamini juu ya Mungu mmoja, aliyeko katika nafsi tatu, yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
2. Linaamini kuwa neno la Mungu yaani Biblia, ndilo pekee lililo na mamlaka ya mwisho katika maisha ya mwamini.
3. Linaamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu aliyezaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na bikira Mariamu.
4. Linaamini juu ya kuishi kwa Yesu bila kutenda dhambi pamoja na miujiza aliyotenda kama ilivyoonyeshwa katika Biblia takatifu.
5. Linaamini kifo cha Yesu pale msalabani kwa ajili ya dhambi za ulimwengu mzima, kufufuka kwake kwa ushindi na kupaa kwake.
6. Linaamini juu ya kubariki watoto wadogo pamoja na ubatizo wa maji baada ya kuamini, unaofanyika kwa kuzamishwa majini, katika jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
7. Linaamini juu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu unaodhibitishwa na ishara ya kunena kwa lugha pamoja na bidii katika kuifanya kazi ya Mungu.
8. Linaamini juu ya uponyaji wa kitabibu pamoja na ule wa kimiujiza kutoka kwa Mungu.
9. Linaamini juu ya ndoa takatifu inayopata baraka kanisani kati ya mke na mume.
10. Linaamini juu ya Ufufuo wa wenye haki, kabla ya kunyakuliwa kwa kanisa. Linaamini juu ya kunyakuliwa kwa kanisa, kutakaotokea kabla ya kuanza kwa kipindi cha dhiki kuu.
11. Linaamini juu ya kurudi kwa Yesu mara ya pili akiwa na watakatifu baada ya dhiki kuu na kutawala duniani kwa kipindi cha miaka 1000.
12. Linaamini juu ya hukumu ya mwisho, ambapo Ibilisi atatupwa katika Jehanamu ya moto pamoja na wote waliokataa kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.
13. Linaamini juu ya ufufuo wa wasioamini, utakaotokea muda mfupi kabla ya hukumu ya mwisho.

 

 

Events Rodrick2 Pokea muujiza

Jesus is Lord and Savior

SHUHUDA ZA AJABU
MIUJIZA HAPA

Kwa miaka zaidi ya 20 kanisa la Maranatha Reconciliation limekekuwa likimwakilisha Yesu Kristo kwa kutekeleza agizo kuu la utume alilotuachia, ambapo pamoja na kuhubiri Injili limekuwa likiombea watu walioonewa na shetani kwa kuponya magonjwa, kutoa pepo na nguvi zote za. SOMA SHUHUDA HAPA.

Kwa mawasiliano

Usisite kuwasiliana nasi wakati wowote kwa kutumia anwani na simu zifuatazo:-

Posta: P.O. Box 7812, Dar es Salaam
Simu: +255 719 310021
Others: +255 655 855 553
Email: maranathainfo@maranatha-upendo.org

© Copyright Maranatha Reconciliation Church (MRC), Tanzania Design by Integrity Marketing Communications