MASWALI NA MAJIBU

Katika ukurasa huu unaweza kuuliza swali lolote linalohusiana na imani ya Ukristo; kama ni kuhusu Biblia, maisha ya kila siku ya kiroho au huduma au historia ya kanisa na kadhalika. Kanisa la Maranatha Reconciliation linaamini kwamba mwamini asiyekuwa na uelewa wa kutosha wa neno la Mungu au mafundisho ya Biblia hawezi kuwa na maisha yenye ushindi aliyotuitia Mungu, na maendeleo ya mwamini wa aina hii huwa ni magumu. Ni wale waamini walio na maarifa ya kutosha ya neno la Mungu ndiyo watakaoweza kuhimili mawimbi yanayoikumba dunia ya leo nahatimaye kuumaliza mwendo kishujaa. Askofu Rodrick Rodrick Mbwambo Mungu amekuwa akimtumia kwa miaka zaidi ya 20 sasa kuhudumu kama mwalimu wa neno la Mungu. Yeye binafsi, kutokana na kiu kubwa ya kumjua Mungu baada ya kuokoka aliamua kwenda chuo cha Biblia ambapo alipata mafunzo zaidi ya elimu ya Mungu. Watu wengu wameweza kumjua Mungu vizuri zaidi kupitia huduma yake ya ualimu na ushauri. Sasa, kwa msaada wa Roho Mtakatifu yuko tayari kujibu maswali yanakuitatiza. Haijalishi hata kama unalelewana mchungaji mwingine, sisi sote ni mwili mmoja na Mungu ametuita ili tushirikishane zawadi. Zingatia majibu ya maswali mengine yamejibiwa na watumishi wengine wa Mungu na tumeona tufanye hivyo kwa kuwa kanisa hili linaamini kumtuikia Mungu kama mwili wa Kristo. Mungu akubariki. Unaweza kutuma swali lako kwa kujaza fomu hapo chini.

Baadhi ya Maswali yenye Utata na
yanayoulizwa mara kwa mara

"Je, Yesu ni Mungu? Je, Yesu alitoa madai ya kuwa yeye ni Mungu?"
"Je, ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo?"

"Je, biblia kweli ni neno la Mungu?"




Swali: "Je, Yesu ni Mungu? Je, Yesu alitoa madai ya kuwa yeye ni Mungu?"


Jibu:
Yesu hakunakiliwa mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?

Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!

Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”

Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote w (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti. Limejibiwa na: www.gotquestions.org/kiswahili




Swali: "Je, ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo?"

Jibu:
Je ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo? Sehemu muhimu katika Bibilia inyo jibu swali hili ni Yohana 3:1-21. Bwana Yesu Kristo akizungumza na Nikodemo mkuu kati ya mafarisayo na mfuasi katika kikao (mahakama) kikuu cha wayahudi (Mfalme wa wayahudi). Nikodemo alikuwa amemjia Yesu usiku. Nikodemo alikuwa na maswali ya kumuuliza Yesu.

Wakati Yesu akizungumza na Nikodemo, alisema, Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?” “Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu, “Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili…” (Yohana 3:3-7).

Msemo “kuzaliwa mara ya pili” unamaanisha “zaliwa toka juu” Nikodemo alikuwa na uhitaji wa kweli. Alihitaji mabadiliko ya moyo wake... Mabadiliko ya kirohoUzao mpya, kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo au hatua ya Kiungu ambapo uzima wa milele hupewa mtu yule aaminiye (2Wakorintho 5:17; Tito 3:5; 1Petro 1:3; 1Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1-4, 18). Yohana1:12, 13 inasema ya kuwa”kuzaliwa mara ya pili” pia ina maana “kufanyika mtoto wa Mungu”kwa imani katika jina la Yesu Kristo.

Swali hasa ni kuwa, “kwa nini mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili?” Mtume Paulo katika Waefeso 2:1 asema, “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi …” Kwa Warumi katika Warumi3:23, Mtume aliandika, ”kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. “Kwahivyo mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili ili asamehewe dhambi zake na awe na uhusiano na Mungu.

Je, hii hutokea vipi? Waefeso2:8, 9 yasema, kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu.” Mtu anapo “okolewa”, basi yeye amezaliwa mara ya pili, akijazwa upya kiroho, na sasa amefanyika kuwa mwana wa Mungu kwa haki ya uzao mpya. Kwa kumwamini Kristo Yesu, yeye aliye adhibiwa kwa ajili ya dhambi alipokufa msalabani, ndiyo maana ya “kuzaliwa mara ya pili” kiroho. “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya…” (2Wakorintho 5:17 a).

Kama bado hujaweza kumwamini Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, je utakuwa na utayari wa kupokea Roho mtakatifu wakati akizungumza na moyo wako? Unahitaji kuzaliwa mara ya pili. Je, utaomba maombi ya kutubu na ufanyike kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo hivi leo? “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13).

Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako na uzaliwe mara ya pili, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-karama ya uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.o la Mungu? Limejibiwa na: www.gotquestions.org/kiswahili




Swali: "Je, biblia kweli ni neno la Mungu?"


Jibu:
Jibu letu katika swali hili halitagusia tu mtazamo wetu juu ya biblia na umuhimu wake maishani mwetu bali pia hatimaye litakuwa na mguso wa milele maishani mwetu. Kama biblia kweli ni neno la Mungu, basi natulifurahie, tulisome, tulitii na kuliamini. Kama biblia ni neno la Mungu basi kulikataa ni kumkataa Mungu.

Kupatiwa kwetu biblia na Mungu ni kithibitisho cha kuwa Mungu anatupenda. Neno “ufunuo” lina maana ya kuwa Mungu aliwasiliana na mwanadamu jinsi alivyo na ni kwa jinsi gani tunaweza kupata ushirika mwema naye. Haya ni mambo ambayo hatungeweza kuyajua kama Mungu hangekuwa ameyawasilisha kwetu katika biblia. Ijapokuwa ufunuo wa Mungu katika biblia umetolewa kwa mfululizo ndani ya takriban miaka 1500 umehifadhi kila kitu mwanadamu anahitaji kumjua Mungu ili awe na ushirika mwema naye. Kama biblia ni neno la Mungu kweli basi ndiyo mamlaka ya mwisho katika mambo ya kiimani, dini na wema.

Swali ambalo sharti tujiulize ni tunawezaje kujua bibilia ni neno la Mungu wala si kitabu tu? Ni kitu gani maaluum ndani ya biblia ambacho huifanya biblia iwe kitabu maalum mbali na vitabu vyengine vya dini Je, kuna ushahidi kuwa biblia ni neno la Mungu kweli? Haya ndiyo baadhi ya maswali ambayo yanahitajika kuangaliwa kama ni tunahitaji kujua kweli biblia ni neno al Mungu, lilitoka kwake na lenye kujitosheleza katika mambo yote ya kiimani.

Hakuwezi kuwa na shaka katika swala la kuwa biblia ni neno la Mungu. Haya yanapatikana katika aya kama Timotheo wa pili 3:15-17, inayosema, “… Kutoka utotoni mmeyajua maandiko matakatifu, yenye uwezo wa kuwafanya ninyi werevu kwa ajili ya wokovu kupitia imani iliyo katika Kristo Yesu. Maandiko yote yametolewa kwa pumzi ya Mungu na yanafaa kwa mafundisho, kwa kuonya, kwa kurekebisha, kwa kuelekeza katika hakii ili mtu wa Mungu akamilishwe kwa ajili ya kila kazi njema.”

Ili tuyajibu maswali haya kwa usahihi, lazima tutazame ushahidi wa ndani na nje wa kuwa kweli biblia ni neno la Mungu. Ushahidi wa ndani ya biblia ni yale maandiko ambayo yanaelezea kuhusu chanzo cha kuweko kwake. Ushahdi wa kwanza ni katika ule umoja wake biblia. Ingawa ina vitabu sitini na sita vilivyoandikwa katika mabara matatu kwa lugha tatu tofauti ndani ya takriban miaka 1500 na waandishi zaidi ya 40 (waliotoka katika taaluma mbalimbali), biblia inabaki kitabu chenye kuhifadhi umoja kutoka mwanzo mpaka mwisho bila kujipinga chenyewe. Hali hii ni maalum kulinganisha na vitabu vyengine na inathibitisha kuweko kwa sauti ya Mungu ikinakiliwa na wanadamu.

Lengine katika ushahidi wa ndani, lapatikana katika unabii ulioorodheshwa ndani ya kurasa za biblia. Humu tunapata unabii juu ya mataifa binafsi kama vile Israeli, unabii wa miji Fulani, unabii wa maisha ya wanadamu na hata wa kuja kwake masihi, mwokozi si wa Israeli tu bali hata kwa wale pia watakaomwamini. kinyume cha unabii unaopatikana katika vitabu vyengine ama ule uliofanywa na Nostradamus, unabii wa kibiblia unatimia. Kuna unabii zaidi ya mia tatu kuhusu Yesu kristo katika Agano la kale pekee. Haikutabiriwa tu atazaliwa wapi na atakuwa wa jamii gani lakini pia ya kuwa angekufa na kufufuka siku ya tatu. Hakuna njia mwafaka ya kuelezea ni kwa uwezo gani unabii huu ulitimizwa ispokuwa kukiri ni kwa uwezo wa Mungu. Hakuna kitabu chenginecha dini chenye unabii unaodhihirika kama Biblia.

Ushahidi wa tatu unapatikana katika uweza na mamlaka ya Biblia. Hili si jambo dogo la kupuuzwa. Biblia ina mamlaka kuliko vitabu vyovyote vyengine. Uwezo huu unaonekana katika maisha ya wanadamu kama vile watu wasiohesabika wameweza kubadilishwa kwa kusoma biblia. Wenye kutumia mihadharati wameponywa na biblia, wahalifu sugu pia wamebadilishwa na biblia, wenye dhambi hukaripiwa na biblia na chuki kubadilishwa kuwa upendo kwa kulisoma biblia. Biblia ina uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu kwa kuwa ni neno la Mungu.

Mbali na ushahidi wa ndani ya biblia, kuna ushahidi wa nje ya biblia unaothibitisha kuwa biblia kweli ni neno la Mungu. Umakini wa historia kama inavyoelezewa katika biblia ni ushahidi pia. Kupitia watafiti wa mabaki ya vitu vya kale na vitabu vyengine vilivyoandikwa, ratiba ya kihistoria katika biblia imehakikishwa mara kwa mara kuwa ya kweli. Watafiti hao pamoja na majarida wanayoyaandika husema ya kwamba biblia ndicho kitabu chenye kuongoza vyema katika historia sahihi ya maeneo mbalimbali. Jinsi biblia ilivyohifadhi histiria sahihi ya vizazi mbalimbali ni thibitisho ya kuwa ni kitabu cha ukweli pia katika kushughulikia maswala ya dini na mafundisho yake. Hili pia huthibitisha ya kuwa hili kweli ni neno la Mungu.

Jambo lengine ni kwamba heshima ya waandishi wa habari hizi za biblia. Mungu aliwatumia watu wa tabaka mbalimbali kuandika habari hizi. Tukuchunguza maisha ya watu hawa na ya kwamba walikuwa tayari hata kufa kwa ajili ya uaminifu wao kwa Mungu kwa ajili ya yale waiyoyaamini; Inathibitisha kuwa, watu hawa wanyonge na waaminifu walikuwa na uhakika kwamba Mungu kweli alikuwa amezungumza nao. Wale waliondika agano jipya na mamia ya waumini wengine (Wakorintho wa kwanza 15:6) walijua ukweli wa ujumbe wao kwa kuwa walikuwa wamemuona na kushirikiana na Yesu kristo baada ya kufa. Mabadiliko ya kumuona kristo aliyefufuka yalipokewa na uzito mkuu na watu hawa. Walibadilika kutoka kwa uoga wa kujificha na kuwa watu ambao hawaogopi kufa kwa ajili ya ujumbe wa Mungu uliokuwa umefunuliwa kwao. Maisha yao na vifo vyao vinathibitisha ya kwamba kweli biblia ni Neno la Mungu.

Ushahidi mwengine ni katika ile hali ya kutokuharibiwa kwa biblia. Kwa sababu ya umuhimu wake na kwamba ni neno la Mungu, biblia imepitia mapambano hatari mengi katika majaribio ya kuliharibu biblia kuliko kitabu chochote chengine katika historia Kutoka watawala wa jadi wa kirumi kama Diocletian, kupitia madikteta wa kikomiunisti na wale wasioamini kuna Mungu wanaoisho siku hizi, biblia imedhibiti hali yake na kudumu zaidi ya wapinzani wake. Hata sasa ndicho kitabu kinachochapishwa kwa wingi duniani.

Vizazi vyote na nyakati zote duniani,wapinzani wamekuwa wakipuuza biblia na kusema ni hadithi tu za watu lakini watafiti wa kihitoria wadumu wakithibitisha ya kuwa biblia ni kitabu cha kweli. Pia wapinzani wake wameshutumu mafundisho yake kuwa ya kijadi nayaliyopitwa na wakati lakini wema wake na mfumo wake wa kisheria umekubalika katika jamii na mila mbalimbali duniani kote. Inaendelea kushambuliwa na sayansi, saikologia, na vyama vya kisiasa na bado biblia inabaki na umuhimu sawa na ule iliyokuwa nao wakati ikiandikwa. Ni kitabu kilichobadilisha maisj\ha na tamaduni kwa muda wote wa miaka 2000 iliyopita. Haijalishi wapinzani wake wanapambana ki vipi, biblia inabaki ikiwa ni kitabu chenye nguvu, kweli na umuhimu sawa na ule kilichokuwa nao kabla kupigwa vita. Kuhifadhika kwa hali yake ya asili hata baada ya mashambulizi haya yote ni ishara ya kuwa biblia ni neno la Mungu. Isitushangaze ile hali ya kuwa bilia inapigwa vita na kuibuka bado mshindi bila madhara yoyote. Kumbuka Yesu alisema, “ Mbingu na dunia vitapita, lakini neno langu halitapita kamwe” (Marko 13:31). Baada ya kupitia ushahidi huu mtu bila shaka anaweza kusema “kweli Biblia ni Neno la Mungu.” Limejibiwa na: www.gotquestions.org/kiswahili

 

 

 

 

 

 

Events Rodrick2 Pokea muujiza

Jesus is Lord and Savior

SHUHUDA ZA AJABU
MIUJIZA HAPA

Kwa miaka zaidi ya 20 kanisa la Maranatha Reconciliation limekekuwa likimwakilisha Yesu Kristo kwa kutekeleza agizo kuu la utume alilotuachia, ambapo pamoja na kuhubiri Injili limekuwa likiombea watu walioonewa na shetani kwa kuponya magonjwa, kutoa pepo na nguvi zote za. SOMA SHUHUDA HAPA.

Kwa mawasiliano

Usisite kuwasiliana nasi wakati wowote kwa kutumia anwani na simu zifuatazo:-

Posta: P.O. Box 7812, Dar es Salaam
Simu: +255 719 310021
Others: +255 655 855 553
Email: maranathainfo@maranatha-upendo.org

© Copyright Maranatha Reconciliation Church (MRC), Tanzania Design by Integrity Marketing Communications