Wiki hii Maranatha
Somo la leo:
Maisha ndani ya Edeni na anguko (imerudiwa)

BAADA ya Mungu kuwaumba wanadamu, aliwatengenezea bustani na akawaweka ndani ya bustani hiyo. Inawezekana kuwepo kwa bustani hiyo katika nchi ya Edeni, ndiko kulikoisababishia kuitwa bustani ya Edeni. Basi BWANA Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemwumba (Mwanzo 2:8).

WAJIBU NDANI YA BUSTANI YA EDENI  

Kitu cha kwanza ambacho Mungu aliwapa wanadamu baada ya kuwaweka katika bustani yake, ni wajibu. Wajibu huu ulikuwa na mambo makubwa mawili, kuilima na kuitunza bustani hiyo. BWANA Mungu akamchukua huyo mtu akamweka kwenye bustani ya Edeni ailime na kuitunza (Mwanzo 2:15. Kwa kuwa wakati huo kulikuwa hakuna magugu wala kitu chochote kinachoweza kuharibu mazao, ni wazi wajibu huu ulikuwa unamaanisha, kuiendeleza bustani hii hadi ifunike nchi yote ya Edeni.

Wajibu huu, unatuonyesha jinsi Mungu anavyofanya kazi, huteua kitu kidogo ili kizae kitu au jambo lililo na ukubwa wa kushangaza. Alipandikiza bustani ndogo kwa ajili ya mwanadamu na kumtaka aiendeleze katika nchi yote ya Edeni. Kutokana na ukweli huu, kama unafanya jambo lo lote linaloufurahisha moyo wa Mungu, jambo hilo litapanuka na kuwa kubwa, hata kama kwa sasa linaonekana kuwa dogo.

Jambo lingine, tunalojifunza katika maandiko haya, ni umuhimu wa kuwajibika katika ufalme wa Mungu. Kuwajibika, ni kwa muhimu sana katika uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Baadhi ya watu wanadhania kuwa kufanya kazi ni adhabu iliyotokana na uasi uliofanywa na Adamu na Eva. Andiko letu hapo juu, halikubaliani na dhana hii. Baada ya Mungu kufanya kazi kwa siku sita, aliwataka wanadamu aliowaumba, nao wafuate nyayo zake kwa kufanya kazi. Mungu ni mchapa kazi, hivyo anahitaji kushirikiana na watu wanaofanya kazi kwa bidii.

Soma zaidi..

 

Events Rodrick2 Pokea muujiza

Habari ya leo: Semina ya Kitaifa, Dar es Salaam

Kwa mara nyingine tena kanisa la Maranatha Reconciliation Church linakuletea semina kubwa ya kitaifa ya kila mwaka itakayofanyika kuanzia tarehe 10 Oktoba hadi 16 Oktoba, 2011, kwenye makao makuu ya kanisa jijini Dar es Salaam.

Katika semina hii ya ajabu, mhubiri wa kimataifa ndugu Ben Hanegraaff kutoka Uholanzi atakuwepo kuhudumu neno la Mungu. Hali kadhalika wahubiri kutoka Kenya watafundisha neno la Mungu wakishirikiana na baadhi ya walimu kutoka Tanzania.

Mtumishi wa Mungu Ben Hanegraaff anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 30 Septemba, 2011 ambapo yeye pamoja na mwenyeji wake Askofu Rodrick Mbwambo wataanza safari ya semina hii mikoani, Tanzania Bara, kabla ya kumalizia jijini Dar es Salaam.

Pamoja na vipindi vya neno la Mungu visivyopungua vitano kwa siku, ambapo kipindi kimoja kitakuwa kikifanyika usiku, pia kutakuwa na warsha za aina mbalimbali kama vile Ujasiriamali, Akina Mama, Vijana, n.k.

Inatarajiwa katika semina hii kuwepo kwa uimbaji usio wa kawaida wa sifa na kuabudu, kwaya pamoja na waimbaji binafsi ambao kwa pamoja watamwimbia Bwana na kuuvuta uwepo wa Mungu wakati wa semina.

Wanasemina wasiopungua mia mbili wanatarajiwa kuhudhuria semina hii wakitokea mikoani, ambao wataweka kambi kwenye makao makuu ya kanisa. Kwa wanasemina wanaotokea Dar es Salaam hawatapewa malazi, isipokuwa chakula cha mchana tu. Hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri kwa neema ya Mungu.

Huduma ya chakula na vinywaji kama kawaida itatolewa kwa ubora zaidi tofauti na ilivyokuwa katika semina ya mwaka jana.

Askofu Rodrick Mbwambo pamoja na mkewe Grace Mbwambo wanapenda kukualika katika semina hii ya kipekee bila kukosa. Usikose, na mweleze na mwingine. Habari zaidi utaendelea kuzipata pia kupitia


Bookstore
Kipindi cha radio
Pia unaweza kutufuatilia kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter
Facebook Twiter
Sifa na kuabudu
SIFA NA KUABUDU
Online shopping

Jesus is Lord and Savior

SHUHUDA ZA AJABU
MIUJIZA HAPA

Kwa miaka zaidi ya 20 kanisa la Maranatha Reconciliation limekekuwa likimwakilisha Yesu Kristo kwa kutekeleza agizo kuu la utume alilotuachia, ambapo pamoja na kuhubiri Injili limekuwa likiombea watu walioonewa na shetani kwa kuponya magonjwa, kutoa pepo na nguvi zote za. SOMA SHUHUDA HAPA.

Kwa mawasiliano

Usisite kuwasiliana nasi wakati wowote kwa kutumia anwani na simu zifuatazo:-

Posta: P.O. Box 7812, Dar es Salaam
Simu: +255 715 310021
Others: +255 655 855 553
Email: maranathainfo@maranatha-upendo.org

© Copyright Maranatha Reconciliation Church (MRC), Tanzania Design by Integrity Marketing Communications

Online shopping